Thursday, March 20, 2008



Gadaffi National Mosque

finally opened


RODNEY MUHUMUZA

KAMPALA

THE Gadaffi National Mosque was opened yesterday amid chaotic supremacy battles between Libyan and Ugandan security officials.

The last of those battles played out at an entrance to the mosque, where President Yoweri Museveni watched in bewilderment as his guards battled the Libyans.

Yet it was only seconds after Libyan leader Muammar Gadaffi had, to sounds of Allah Akbar, lifted a curtain from a memorial monument to officially open the mosque, his gift to Ugandan Muslims.

With his back to the wall, minutes after Col. Gadaffi had entered the mosque, Mr Museveni and Prime Minister Apolo Nsibambi watched as reporters, diplomats and security officials created a melee that would have shocked the Muslims who had already entered the mosque in anticipation of the arrival of at least seven heads of state. By 4pm, thousands had already entered the mosque, and hundreds more watched from the mosque’s fringes as Col. Gadaffi and Mr Museveni made their way inside.

In his speech, Mr Museveni praised Col. Gadaffi for building the mosque “in a record time of three years”, while Col. Gadaffi spoke of the supremacy of Islam, his favourite subject.

cover2_4.jpg
Magnificent: Some of the people who turned up for the opening. Photo by Geoffrey Sseruyange

The mosque, atop Old Kampala hill, was a meeting place for all sorts of people, including a salesman who distributed flyers saying “the United States has reached where it reached today based on deceit”.

Old women were seen carrying photos of “Brother Leader Gadaffi”, drawn from their purses, and they cried out in excitement whenever his name was called out on the microphone.
It was also a day for some Muslims to praise Idi Amin; one Muslim leader, for example, claimed the opening of the mosque was a realisation of Amin’s dream.

In 1972, shortly after coming to power, President Idi Amin donated 12 acres of land at Old Kampala hill to the Uganda Muslim Supreme Council, but efforts to build a mosque there stalled until 2001 when a delegation of Ugandan Muslims travelled to Libya to ask for Col. Gadaffi’s help.

The Libyan leader, through the World Islamic Call Society, financed the construction, although the actual cost remains a mystery.

“It is the biggest mosque south of Morocco,” said Electoral Commission chief Badru Kiggundu, who chaired the construction committee.

“It is the biggest mosque in black Africa.” With its unique architectural style, the mosque will be an object of attraction for many years to come. It can accommodate over 15,000 worshipers in both its open and enclosed space, Prof. Kiggundu said, adding that it is the second largest in Africa after the Hassan II mosque in Casablanca, Morocco.






Karume ashiriki chakula

ufunguzi wa Msikiti Mkuu




Mwandishi Maalumu, Uganda

Daily News; Thursday,March 20, 2008 @00:04


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume juzi jioni aliungana na viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa Msikiti Mkuu nchini humo.

Hafla hiyo ilifanyika Ikulu mjini Entebbe na ilihudhuriwa na viongozi hao akiwamo Rais wa Libya, Muammar Al Gaddafi ambaye ndiye mdhamini wa msikiti huo mkubwa katika eneo la nchi zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara uliojengwa mjini Kampala.

Akiwakaribisha viongozi mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo, Rais Museveni alitoa shukrani zake za dhati kwa ujio wa viongozi hao pamoja na kumpongeza Rais Karume kwa kujumuika pamoja katika hafla hiyo sambamba na uzinduzi wa msikiti huo. Rais Karume alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete, naye alipokea shukrani hizo.

Akizungumza na viongozi hao, Rais Museveni alitoa shukrani zake kwa Rais Gaddafi kwa ujenzi wa msikiti huo mkubwa ambao unaonyesha ishara kubwa ya upendo kati ya wananchi wa viongozi wa Uganda na ndugu zao wa Libya.

Rais Museveni alisema msikiti huo utaimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizo na kusisitiza kuwa Uganda na Libya zina urafiki na udugu wa siku nyingi. Alisema Waislamu wa Uganda wamefarijika kwa kiasi kikubwa kutokana na msaada wa Rais Gaddafi alioufanya kwa kuwajengea msikiti huo wa aina yake.

Alisema msikiti huo ambao ulianzishwa na Rais Iddi Amin mwaka 1972, utasaidia zaidi kuwaunganisha Waislamu wa Uganda na hata Waislamu kutoka nchi nyingine za ndani na nje ya Afrika.

Naye Rais Gaddafi alisema ana furaha kubwa kuona uhusiano na ushirikiano wa Uganda na Libya pamoja na nchi nyingine za Afrika, unaimarishwa kwa kujenga misingi imara ya umoja katika nyanja mbalimbali ikiwamo kuimarishwa kwa dini ya Kiislamu nchini Uganda.

Alisema Libya nayo inathamini uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya nchi za Afrika; na kufurahishwa kwa kuungana pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo akiwamo Rais Karume, Rais Ismail Omar wa Djibouti, Rais Abdilahi Yussuf Ahmed wa Somalia, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi pamoja na viongozi wengine. Msikiti huo ulitarajiwa kuzinduliwa rasmi jana na Rais Gaddafi.




No comments: