Thursday, March 20, 2008

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO VA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa anapenda kuwatangazia Watanzania wenye sifa kutoka Bara na Visiwani, kuomba kazi zilizotangazwa hapa chini. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano .wa Kimataifa inazingatia usawa wa kijinsia katika kutoa ajira. Hivyo wamawake wenye sifa wanahimizwa kuomba.

Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:­

1. AFISA MAMBO VA NJE MKUU DARAJA LA I, TGS H (NAFASI 2)

KAZI ZA KUFANYA

i. Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje kwa kutilia maanani masuaJa yaliyopewa kipaumbele katika kukuza na kuimarisha uchumi wa Taifa.

ii. Kufanya tathmini za utekelezaji wa Sera mbalimbali za kiuchumi na kutoa ushauri na mapendekezo ya utekelezaji wake.

iii. Kuratibu Wizara na Taasisi mbalimbali kutekeleza majukumu/makubaliano yaliyokubalika Kikanda na Kitaifa (Regional and International Cooperation) kwa wakati uliokubalika.

SIFA ZA MWOMBAJI

i. Awe na Shahada ya Uzamili (Masters) kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani zifuatazoa.

a. Uhusiano wa Kimataifa

b. Public Policy

c. Uchumi

d. Biashara ya Kimataifa; na

e. Sheria ya Kimataifa.

ii. Awe na ujuzi wa kutumja kompyuta pamoja na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka kumi na mbili (12).

SIFA ZA ZIADA

Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile, Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani, Kihispania na Kiarabu.

2. AFISA MAMBO YA NJE MWANDAMIZI, TGS F (NAFASI 1)

KAZI ZA KUFANYA

i. Kuhudhuria mikutano ya Kimataifa.

ii. Kutafiti na kuchambua taarifa mbalimbali.

iii. Kuratibu njia za wageni toka nje zinazopitia Anga za Nchi yetu au kutua nchini.

iv. Kuratibu mabaraza ya pamoja ya ushirikiano baina ya nchi yetu na Mataifa ya nje.

v. Usaili katika ngazi za Kiwaziri na Kibalozi.

SIFA ZA MWOMBAJI

i. Awe na Shahada ya Uzamili (Masters) kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani zifuatazo:

a. Uhusiano wa Kimataifa;

b. Public Policy;

c. Uchumi;

d. Biashara ya Kimataifa; na

e. Sheria ya Kimataifa.

ii. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka saba (7).

SIFA ZA ZIADA

Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani, Kihispania na Kiarabu.

3. AFISA MAMBO VA NJE DARAJA LA II, TGS D (NAFASI 8)

KAZI ZA KUFANYA

I. Kuandaa Muhtasari, nakala na taarifa zinazohusu masuala ya mahusiano ya Kimataifa.

II. Kuhudhuria mikutano mbalimbali.

III. Kuandaa mahojiano.

IV. Kufuatilia masuaJa mbalimbali ya kimataifa.

V. Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbali yanayohusu uchumi, siasa na jamii.

VI. Kutunza kumbukumbu za matukio mbalimbaJi. .

SIFA ZA MWOMBAJI

Awe na Shahada ya Sanaa (B.A.) kutoka Chuo (kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali, na ambaye amejiimarisha (major) katika mojawapo ya fani zifuatazo:­

a. Uhusiano wa Kimataifai

b. Uchumi; na

c. Sheria.

ii. Awe amefanya na kufaulu mtihani unaotolewa na Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam.

iii. Awe na ujuzl wa kutumia kompyuta.

SIFA ZA ZIADA

i. Awe mwenye uwezo wa kuzungumza Jugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kireno Kirusi, Kichina, Kijerumani, Kihispania na Kiarabu.

ii. Mwenye Shahada/Stashahada ya Uzamili (Masters/Postgraduate Diploma) kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na SerikaJi katika mojawapo ya fani zifuatazo:­

a. Uhusiano wa Kimataifa;

b. Public Policy;

c. Uchumi;

d. Biashara ya Kimataifa; na

e. Sheria ya Kimataifa.

4. AFISA TAWALA MWANDAMIZI, TGS F (NAFASI 7)

KAZI ZA KUFANYA

i. Kuandaa bajeti ya matumizi ya Wizara.

ii. Kuratibu na kuhifadhi kumbukumbu za matukio muhimu katika Wizara.

iii. Kufanya kazi za uhusiano na itifaki Serikalini. Kushughulikia masuala ya nidhamu na ufanisi wa kazi kwa watumishi wa Wizara.

iv. Kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo kulingana na mahali alipo.

v. Kuandaa taarifa za utendaji na matukio mbalimbali kila mwezi.

vi. Kutekeleza utaratibu wa uundwaji na utendaji wa Mabaraza ya Wafanyakazi kwa mujibu wa kanuni na taratibu.

SIFA ZA MWOMBAJI

i. Awe mwenye Shahada/Stashahada ya Uzamili (Masters au Postgraduate Diploma) kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katiko Fani zifuatazo:­

a. Utawala;

b. Elimu ya jamii;

c. Sheria (baada ya internship);

d. Menejimenti Umma; na

e. Uchumi.

ii. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka saba (7). Aidha, mafias tawala watakaoajiriwa katika cheo hiki watatakiwa kufanya au kufaulu mtihani wa maafisa tawala katika kipindi cha miaka miwili tangu waajiriwe.

SIFA ZA ZIADA

Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani, Kihispania na Kiarabu.

5 KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III, TGS B (NAFASI 2)

KAZI ZA KUFANYA

i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.

ii. Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kudhughulikiwa.

iii. Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.

iv. Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi Wizarani.

v. Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.

vi. Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kukusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.

SIFA ZA MWOMBAJI

i. Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kuhudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu.

ii. Awe amefaulu soma la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa daika moja na awe amepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

SIFA ZA ZIADA

Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani, Kihispania na Kiarabu.

MASHARTI KWA WAOMBAJI WOTE: ­

1) Maombi yaandikwe kwa mkono na kuambatanishwa nakala za vyeti vya Shule, Vyuo, Vyuo Vikuu (Certificate and transcript) na kozi uJizohudhuria.

2) Wasifu binafsi wa mwombaji (CV) pamoja na picha moja ya

pasipoti ya siku za karibuni.

3) Kwa wale wote walioajiriwa maombi yao ya kazi ni lazima

yapitishwe kwa waajiri wao.

4) Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 45.

5) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi vote ni Februari 29,

2008.

Maombi vote yatumwe kwa anuani ifuatayo:­

Katibu Mkuu

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

S.L.P.9000

DAR ES SALAAM.


No comments: