Friday, March 21, 2008

Maimartha anauza dawa za

kuongeza makalio na matiti



Mtangazaji maarufu wa Kituo cha Televisheni cha EATV cha jijini Dar es Salaam, Maimartha Jesse, anashutumiwa kuyaweka hatarini maisha ya wanawake wenzake nchini kufuatia kudaiwa kuuza dawa za kuongeza makalio na matiti....

Maimartha


Taarifa zilizolifikia gazeti hili zilidai kuwa, katika duka la mwanadada huyo mwenye makeke awapo katika kipindi chake cha Afro-Beat, lililopo Kinondoni, anauza sabuni na dawa zinazoweza kumfanya mwanamke kuongeza makalio na matiti.

Hata hivyo, taarifa hizo zimepokelewa ndiyo sivyo na baadhi ya wataalam wa afya ambao wametahadharisha kuwa wanaotumia dawa hizo hawajipendi.

Mmoja wa madaktari maarufu jijini Dar es Salaam aliyeomba hifadhi ya jina lake alieleza kuwa, kitendo cha Maimartha kuwauzia wanawake dawa hizo ni kuwaweka katika mazingira ya kuathirika kiafya.

Alisema, wanaouza dawa hizo huenda hawajui madhara yake kwani zina uwezo mkubwa wa kuharibu mfumo wa vichocheo vya mwili ‘hormones’, hivyo kuweza kumsababishia mwanamke kuzeeka haraka na kuathiri vichocheo vinavyohusika na mfumo wa mambo ya uzazi.

“Mwanamke anayetumia dawa hizo hujiweka katika mazingira ya kupata kansa, ugonjwa ambao umepoteza maisha ya baadhi ya watu. Niseme tu kwamba wanawake wakiendelea kuwa na tamaa ya kuwa na maumbile ambayo hawakuumbwa nayo, maisha yao yatakuwa mafupi,” alitasema Daktari huyo.

Kutoka gazeti la Amani.



1 comment:

Anonymous said...

JAMANI KWANI TATIZO LIKO WAPI?
WATEJA HUNUNUWA WENYEWE;ILI MRADI HAIBI CHA SERIKALI SAWA KABISA: TUANDIKE MAMBO YA MAANA KAMA UFISADI NA KADHALIKA: HATA SALOON RUKUSA KUUZA NGONO