Wednesday, March 26, 2008


Mambo Yanaendelea
Comoro..

Picha ya chini ni Wanajeshi wa jeshi la wananchi la Tanzania(JWTZ) wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi wapiganaji kutoka kundi la waasi linaloongozwa na Colonel Mohamed Bacar ambaye inasemekana hajaonekana kisiwani hapo kwa siku tatu sasa.Hata hivyo majeshi kutoka africa Union yakiongozwa na jeshi la wananchi wa Tanzania yameanza msako mkali wa kumtafuta kiongozi mkuu wa waasi Col Mohamed Bacar baada ya kutwaa mji mkuu Anjouan na Uwanja wa ndege mapea jana.Hata hivyo habari za kuaminika kutoka Comoro zinasema wapiganaji Saba wa Col Mohamed Bacar wameuawa mpaka sasa huku kukiwa hakuna vifo wa majeruhi kutoka vikosi vya Africa Union vikiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania..

kutoka: http://haki-hakingowi.blogspot.com/


JWTZ wachukua Anjouan


Wanaume wakiingia mji mkuu wa Anjouan, Mutsamudou.


Habari za uhakika zinasema kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likiongoza vikosi vya Umoja wa Afrika (AU) vimeuteka mji mkuu wa uwanja wa ndege wa Anjouan na kuwa hakuna askari yeyote wa JTWZ aliyejeruhiwa au kuuawa. Hapa wanajeshi wa JWTZ wakiwa mitaani
Mutsamudou na wakishangiliwa na wananchi.

Habari na picha toka BBC/AFP. Zaidi BOFYA HAPA


No comments: