Sunday, March 09, 2008

Mwanae Salmin

atupwa rumande


Na Hellen Mwango

Mtoto wa aliyekuwa rais wa Zanzibar, Salmin Amour, amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kujipatia Dola za Marekani 6,000 kwa njia ya udanganyifu.

Mshtakiwa huyo Amini Salmin Amour (36), anashtakiwa na mwenzake Manir Juma (35), ambao walipelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti.

Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Mkazi Rose Kangwa.

Inspekta Msaidizi wa Polisi Edwin Boniface, alidai kuwa mwezi Februari mwaka huu jijini Dar es Salaam washtakiwa walikula njama kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa Februari mosi mwaka huu eneo la Mikocheni A, jijini Dar es Salaam washtakiwa walijipatia Dola za Marekani 6,000 kutoka kwa Baosheng Ge baada ya kumdanganya kuwa wangempangisha kwenye nyumba iliyo kwenye ploti namba MKC/MCA/207 eneo la Mikocheni huku wakijua kuwa si kweli.

Washtakiwa walikana shtaka hilo na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya wadhamini wawili walioajiriwa serikalini na watakaosaini bondi ya Shilingi milioni saba.

Kesi imeahirishwa hadi Machi 19, mwaka huu.Wakati huo huo katika mahakama hiyo mkazi wa jijini Dar es Salaam, Ismail Selemani (29), anakabiliwa na shtaka la wizi.

Mshtakiwa alisomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Rose Kangwa.

Ilidaiwa kuwa Januari 5, mwaka huu eneo la Kinondoni Mkwajuni, mshtakiwa aliiba mkoba wa Minaeri Kasijila uliokuwa na Sh. 930,000, kadi ya benki na kitambulisho.

Mshtakiwa alikana shtaka hilo na kesi yake itatajwa Machi 19, mwaka

Kutoka gazeti la Nipashe.

No comments: