Monday, March 24, 2008

Na Issa Mnally


Wakati Jiji la Dar es Salaam kwa kutumia kada zake za dola, likipambana kikamilifu kuhakikisha linatokomeza biashara ya ukahaba, kama nyenzo ya kuimarisha vita dhidi ya Ukimwi, hali bado ni hatari....

Uwapo wa matukio mengi ya kifuska, wakati wa sherehe za Pasaka, ni hali inayotoa ishara ya wazi kwamba kufanikiwa kuondosha biashara hiyo ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu.

Uchunguzi wa gazeti hili, uliweza kubaini wanawake wengi wanaojiuza (machangudoa) wakiwa kwenye maeneo mengi maarufu kwa biashara hiyo na wakifanya kazi yao bila hofu.

Baadhi ya maeneo hayo ni Sinza Afrika Sana, Barabara ya Kinondoni, Buguruni, Ilala, Manzese Uwanja wa Fisi na katika viunga karibu na Lambo Bar ya Manzese.

Maeneo mengine ni Barabara ya Ohio, Mwananyamala kwa Wahaya, Barabara ya Uhuru, Kariakoo, karibu na maeneo ya Kisuma Bar na Sugar Ray, Temeke, Makutano ya Barabara za Sofia Kawawa na Nkrumah na kadhalika.

Katika kufanya kazi kwa mifano, usiku wa Ijumaa Kuu ambao kwa kawaida ni kumbukumbu ya mateso ya Bwana Yesu msalabani, mmoja wa wanatimu ya dawati la Ijumaa Wikienda, alifanikiwa ‘kumnunua’ changudoa mmoja nje ya Klabu ya Usiku ya Ambiance, iliyopo Sinza.

Aidha, ‘kachero’ wetu, aliombwa na changudoa huyo, kutoa shilingi 7,000 kwa ajili ya huduma ya chapchap (short time).

Baada ya makubaliano hayo, kachero wetu alimpakia mrembo huyo kwenye pikipiki na kwenda naye hadi kwenye nyumba moja (siyo gesti), kama sehemu ya makubaliano.

Hata hivyo, kwa vile lengo lake halikuwa kujamiiana na changudoa huyo, mwandishi wetu alianza kumuuliza maswali mbalimbali kuhusu biashara yao ya kujiuza na changamoto zinazowakabili kwa sasa.

Maswali hayo, hayakuweza kujibiwa na changudoa huyo ambaye alidai anapotezewa muda wa kuwahi kurudi kazini, hivyo aliomba apewe chake mapema, kisha ‘kazi ianze’.

Habari zaidi zinasema kwamba jitihada za mchunguzi wetu, kumbana kwa maswali mwanamke huyo ziligonga ukuta, hivyo aliamua kumpa pesa yake (shilingi 7000) ili kila mtu ashike hamsini zake.

Hata hivyo, changudoa huyo hakukubali kuachwa kwa staili hiyo, badala yake alilazimisha kuwa ni lazima ajivinjari na kachero wetu kama walivyokubaliana.

“Yaani unanileta huku, kuniuliza maswali halafu unanipa hela niondoke. Kumbe wewe ni mwandishi eeeh! Basi leo utachoka na muziki wangu, ni lazima uni… (tusi),” alisema changudoa huyo ambaye hata alipoulizwa jina lake, hakutaja.
Katika kuonesha kwamba hakuwa akitania, changudoa huyo alianza kuvua nguo moja baada ya nyingine, hadi akabaki mtupu kisha akamvaa mwandishi wetu akimlazimisha wafanye mapenzi.

“Mimi sikuelewi, hatujakubaliana unipe hela ya bure, tumekubaliana unipe nikupe. Kama wewe ni mwandishi, leo utakoma kuringa, mimi sichezewi,” alisema kwa kufoka.

Hata hivyo, waandishi wengine wa Ijumaa Wikienda, walifika mara moja kumuokoa mwenzao na varangati hilo na kumtaka changudoa huyo kuondoka kwakuwa alikuwa ameshapewa pesa zake.

Pamoja na hali hiyo, changudoa huyo aliendelea kufanya fujo, mpaka mmoja wa waandishi wetu alipomtishia kumuitia polisi, jambo ambalo lilimtia hofu mwanamke huyo na kutimua mbio akiwa nusu uchi.

Baadhi ya picha za matukio ya mrembo huyo akifanya fujo, zinaonekana ukurasa wa kwanza wa gazeti hili.

Katika hatua nyingine, Makongoro Oging’ anaripoti kuwa jumla ya wanawake 26, wanaojiuza walikamatwa siku chache kabla ya Pasaka, Buguruni, jijini Dar es Salaam.

Warembo hao ambao hujulikana pia kwa jina la wadoezi wa mali za watu, wawili kati yao, wanaonekana ukurasa wa kwanza wa gazeti hili katika picha ndogo chini kushoto.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogire alithibitisha kuwepo kwa kamata kamata hiyo na kuongeza kuwa kazi ya kuwakamata machangudoa bado inaendelea na kwamba itakoma pale akina dada hao watakaposalimu amri.

2 comments:

Anonymous said...

HI JAMANI HAKUNA SHERIA INAYO ZUIA KUTOTOA PICHA YA MTU KAMA UNAVYOFANYA HAPA: HUYU NI BADO MTUHUMIWA NA SI SHERIA KUTOA PICHA YA MTU NAMNA HII:WANASHERIA MNAOTETEA HAKI ZA BINADAM WACHUKULIENI SHERIA MAGAZETI KAMA HAYA:KWANI HUTOA PICHA ZA WALALA HOI HAPA KWA AJIRI YA BIASHARA:KAMA NI NGONO VIONGOZI KIBAO WANA MAJUMBA MADOGO MBONA HAWATOI HAPA TUKAWAONA?

Chama Cha Watanzania Oslo - CCW Oslo said...

Inavyoelekea huko Tanzania sheria hii haipo au kama ipo haitiliwi maanani.