Monday, March 24, 2008

Mungu wangu wee!!



Christopher Lissa na Richard Bukos

Mkazi wa Kijiji cha Kilema kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro, (jina tunalihifadhi) anadaiwa kubambwa ‘laivu’ na mkwewe (mke wa mtoto wake) akiwalawiti wajukuu zake wa kike ambao ni mapacha ndani ya zizi la ng’ombe...

Akizungumza na Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki, mama mzazi wa watoto hao, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Siku ya Wapendanao Februari 14, mwaka huu, ingawa anasikitishwa na familia ya mkwewe kulifumbia macho suala hilo.

Akisimulia ilivyokuwa, mama huyo alisema mara baada ya kujifungua aliondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Moshi, ambapo wakwe zake walimuita ili wakamhudumie na kumfanyia mambo ya kimila.

Alisema katika safari hiyo alifuatana na mumewe Gowi hadi Kilema Moshi na baada ya kuishi huko kwa miezi miwili, mumewe alirudi Dar es Salaam na kumuacha na watoto ukweni.

Alisema, alianza kupata shaka na mkwewe huyo pale alipokuja kufumwa na mkewe akimuingiza vidole kwenye sehemu za siri, mmoja wa watoto hao na alipobanwa aliomba asamehewe kwa madai alipata ushawishi wa kishetani.

“Siku nyingine tena mama mkwe alimfuma mumewe akimuingiza vidole sehemu za siri mtoto mwingine wakati akijisaidia, ndipo mama mkwe ikabidi aitishe kikao cha wazee ili kumkanya mzee huyo,” alisema.

Alidai pamoja na kukanywa lakini Februari 14, mwaka huu mchana wakati akiandaa chakula alisikia kilio cha mtoto wake na alipotoka nje na kumuuliza shemeji yake aliyemtaja kwa jina moja la Roger kuna nini ndipo akaambiwa mkwewe kaingia na watoto kwenye zizi la ng’ombe.

"Ilibidi nitoke mbio ili kwenda kuwaokoa watoto ambapo nilimkuta baba mkwe akiwa mtupu na akimlawiti mmoja wa watoto.

“Nilimkwapua mtoto kutoka mikononi mwake na nilipomchunguza nilikuta ametapakaa mbegu za kiume sehemu za nyuma, huku akiwa na michubuko mingi sehemu za kukalia,” alisema.

Mama huyo alisema, kitu alichofanya ni kumpigia simu mumewe ambapo ilibidi arudi ghafla Kilema na baada ya kikao cha familia walikubaliana kuyamaliza kindugu masuala hayo, huku wakimuonya kutofichua siri hiyo.

Alisema hakuridhika na hali hiyo, kwani watoto wake waliendelea kuishi na majeraha bila kupatiwa matibabu kutokana na kuzuiliwa na wanafamilia kupelekwa hospitali kwa kuhofu mzee wao atakamatwa.

“Nilipoona watoto wangu wanateseka kufuatia kutokwa na vidonda sehemu za siri, nikamlazimisha mume wangu anirudishe nyumbani kwetu Dar es Salaam na alikubali lakini akinipa sharti nisije nikatoboa siri hii kwa ndugu zangu.

“Tulipofika Dar es Salaam akanipeleka kwa mjomba wake Tabata Liwiti na kunionya nisikutane na ndugu zangu, lakini kwa kuwa hali ya watoto ilizidi kuwa mbaya ikabidi nimtoroke na kwenda Buguruni Kisiwani kwa baba mkubwa.

“Nilipofika pale nilimueleza kilichowasibu watoto, ndipo akanishauri twende kutoa taarifa Kituo cha Polisi Buguruni ambapo tulipewa PF3 nikawapeleka wanangu kutibiwa Hospitali ya Amana,” alisema.

Aliongeza kuwa uchunguzi wa madaktari wa Amana uliofanywa Machi 13, mwaka huu ulionyesha watoto hao wameharibiwa sehemu zao za siri na pia kuambukizwa magonjwa ya zinaa.

Mama huyo alisema kwa sasa anataka msaada mkubwa wa kisheria, kwani Polisi Buguruni wamemshauri aende kufungua mashitaka katika kituo kilichopo eneo la tukio.

“Sina uwezo wa kwenda huko na kufungua mashitaka, kwani hata maisha yangu naona hayapo salama, naaomba msaada ili niweze kwenda na kutetea haki za watoto wangu,“ alisema.

Juhudi za kumpata mtuhumiwa ili kusikia kauli yake bado zinaendelea, akipatikana tutaweka wazi majina ya wahusika.

Kutoka Global Publishers TZ.


No comments: