Sakata
Rostam si raia wa Tanzania?
2008-03-17 19:09:42
Na Emmanuel Lengwa, Jijini
Mbunge wa jimbo Igunga, kupitia CCM, Mheshimiwa Rostam Aziz leo amejikuta katika wakati mgumu baada ya taarifa kwamba yeye si raia wa Tanzania kupamba vyombo vya habari mbalimbali.
Alasiri ilipojaribu kupata maoni yake kuhusiana na madai hayo mazito, Bw. Rostam alishtuka kidogo kisha akahoji, ``Wanasema mimi siyo raia...asante sana...asante sana``.
Baada ya kauli hiyo, Bw. Rostam hakutaka kusema tena lolote licha ya kuulizwa mara kadhaa msimamo wake ni upi juu ya madai hayo.
Awali, Alasiri iliwasiliana na Idara ya Uhamiaji kupata ufafanuzi juu ya madai hayo ambapo afisa mmoja wa ofisi ya Uhusiano alisema wanahitaji kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kutoa majibu ya uhalali wa uraia wa Bw. Rostam.
``Naomba unielewe, suala la uraia ni sawa na uhai wa mtu. Hapa mezani kwangu sina nyaraka za kila raia, hivyo inanibidi nipekue mafaili na kuchunguza kwa makini kabla ya kutoa majibu sahihi,`` akasema afisa huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Batenga.
Sakata hilo la uraia limeibuka baada ya mbunge huyo kuhusishwa katika sakata la mkataba tata baina ya Serikali na kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond.
Aliyeibua madai hayo ya sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party, DP, Mchungaji Christopher Mtikila.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini jana, Mchungaji Mtikila alidai Bw. Rostam ni raia wa Iran aliyeingia nchini kama mfanyabiashara wa ngozi.
Akizidi kumshushia madongo mweka hazina huyo wa zamani wa CCM, Mchungaji Mtikila alidai kuwa baada ya kuingia nchini, Rostam hakuwahi kuukana uraia wake na wala hakuwahi kuomba uraia wa Tanzania.
Akasema badala yake, Rostam akajiingiza kwenye siasa moja kwa moja, akisaidiwa na baadhi ya viongozi.
Akizungumza kwa kujiamini, Mchungaji Mtikila akasema sasa, dola lazima imkamate mara moja na kwamba yeye anao ushahidi wa kutosha katika kuthibitisha madai yake.
``Licha ya kuwa Bw. Rostam ni rafiki yangu, siwezi kumtetea yeye kuliko nchi yangu ushahidi wa kuwa yeye sio Mtanzania ninao, maana najua mpaka hospitali aliyozaliwa na mpaka sasa, wazazi wake wako Iran,`` akasema Bw. Mtikila.

- SOURCE: Alasiri
No comments:
Post a Comment