Na Tausi Ally
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, amewasilisha kusudio la kukata rufaa dhidi ya Padri wa Kanisa Katoliki Mlandizi, mkoani Pwani Sixtus Kimaro (38) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kulawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 17.
Kusudio hilo limewasilishwa jana katika Mahakama ya Rufaa Tanzania chini kanuni namba 61 ya Mahakama hiyo ya mwaka 1979.
Hatua hiyo, imekuja baada ya Jaji Justice Makaramba, Machi 14, mwaka huu, kumuachia huru Padri huyo.
Agosti 9, 2006, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, ilimhukumu kutumikia kifungo cha miaka 35 jela, Padri Kimaro kwa kupatikana na hatia ya kulawiti na kushawishi kijana huyo, kumnyonya sehemu zake za siri.
Awali akitoa hukumu hiyo, Khaday alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi nane wa upande wa mashtaka na utetezi wa mshtakiwa huyo, atafungwa kifungo cha miaka 30 jela katika kwa kulawiti na miaka mitano katika shambulio la aibu na kumwamuru kumlipa mvulana huyo, Sh2milioni.
Wakili aliyekuwa akimtetea, Dk Masumbuko Lamwai. aliiomba mahakama impunguzie adhabu mteja wake kwa vile kitendo cha kutiwa hatiani, kimemwondoa katika Upadri kitendo ambacho ni sawa na kifungo cha maisha.
Dk Lamwai aliendelea kuiomba mahakama impunguzie adhabu mteja wake kwa kuwa bado ni kijana anaumia kwa kuwa hata hudumia jamii na kuwa kesi hiyo ilikuwa imetungwa.
Hakimu Khaday hakukubaliana na ombi la Dk Lamwai na kurtoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo.

No comments:
Post a Comment