Na Mwandishi Wetu
Miss Tanzania namba 5, 2005, Irene Uwoya hivi karibuni alijikuta katika wakati mgumu baada ya kudhaniwa kuwa changudoa katika Jiji la Kampala nchini Uganda....

“Kama unavyomfahamu Irene alivyoumbika na tabia yake ya kupenda kuvaa nguo za utata, alipotua mjini humo aliwachanganya wanaume ile mbaya,” kilisema chanzo hicho.
Habari zaidi zilidai kuwa, hivi sasa Irene ni gumzo katika sehemu mbalimbali za burudani nchini Uganda na kuna habari kwamba mfanyabiashara mmoja maarufu anamsaka kwa udi na uvumba.
“Kuna mfanyabiashara amemuaahidi kumnunulia gari na nyumba ya kifahari endapo atakubali kuolewa naye na kubadili uraia,” kilisema chanzo chetu kilicho karibu na mrembo huyo.
Mwandishi wetu alipompigia simu Irene kutaka kujua ukweli wa jambo hili, alithibitisha na kudai kuwa hakutegemea mambo yaliyomkuta Kampala.
“Mimi nilikuwa nahisi waganda wanakwenda na wakati zaidi ya watanzania na vivazi vya utata kwao si jambo la ajabu, kumbe tofauti bwana, jamaa wanahisi mimi malaya na mavazi yangu yanawadatisha kila ninakopita.
“Majuzi kuna mfanyabishara (anamtaja) kanifuata hotelini na kuniahidi kuninunulia gari na nyumba ya kifahari endapo nitakubali kuolewa naye na kubadili uraia niwe Mganda, lakini nimemkatalia,” alisema Irene.
Hivi karibuni mrembo huyo aliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kumtema mwanamuziki H. Baba na kudatishwa na penzi la mzungu.
No comments:
Post a Comment