Watoto wamtapeli
Mama Rwakatare
KATIKA hali isiyotarajiwa, watoto waliojulikana kwa jina moja moja la Yusufu na Ramadhani, wamelidanganya Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God linaloongozwa na Mchungaji Dk. Gertrude Rwakatare, baada ya kujifanya kuwa wamedondoka kutoka angani walikokuwa wakiwanga, kutokana na nguvu ya maombi ya waumini wa kanisa hilo.
Utapeli kuhusu watoto hao, ambao ulitangazwa kwa mara ya kwanza na Kituo cha Televisheni cha ITV, ulithibitishwa kwa gazeti hili na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow, juzi.
Kamanda Rwambow, alisema kabla ya kujifanya wameanguka katika kanisa hilo la Mchungaji Rwakatare, hivi karibuni, watoto hao walifanya jambo kama hilo Januari 6, mwaka huu katika eneo la Tangi Bovu jijini Dar es Salaam.
“Baada ya polisi wangu kupata taarifa za kuanguka kwa watoto hao, walifika eneo la tukio na kuwachukua hadi Kituo Kidogo cha Polisi Kawe na kuwahoji, halafu wakawapeleka Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi wa afya zao.
“Madaktari walichunguza afya zao na kubaini kuwa hawana maradhi yoyote. Lakini jeshi letu lilipata taarifa zaidi kutoka kwa watu wanaowafahamu watoto hao wakisema kwamba, watoto hao ni matapeli,” alisema Kamanda Rwambow.
Aliongeza kuwa, mwanzoni mwa Februari, watoto hao tena walijifanya wameanguka huko Manzese, ambako polisi wa eneo jirani na walipodai kudondoka watoto hao, walifika na kuwachukua.
Kamanda Rwambow, aliongeza kuwa baadhi ya waumini na viongozi wa kanisa moja lililopo Manzese waliwachukua, kuwaombea na kuwapeleka kwenye kituo cha kulelea yatima Kurasini.
Alisema, waumini hao walibaini kwamba watoto hao ni matapeli, waliwaacha na kusisitiza kuwa hao si wachawi wala misukule walioanguka kwa nguvu za maombi kama inavyodaiwa, na kuyatahadharisha makanisa na jamii kuepukana nao pia kuwa makini na matukio ya namna hiyo.
Kabla ya uzushi huo wa aina yake, watoto hao baada ya kubainika na kuwekwa hadharani kwa mara ya kwanza na ITV, waliueleza uongozi wa Kanisa la Mikocheni kuwa walikuwa wakiishi kama misukule katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza kuhusu watoto hao Jumanne wiki hii katika ITV, walezi wao walieleza kuchoshwa na tabia ya utukutu wa Yusufu na Ramadhani wanaokadiriwa kuwa na kati ya miaka saba au 10.
Alipozungumzia suala hilo wakati wa mkutano na waandishi wa habari aliouitisha Machi 17, mwaka huu, Mchungaji Dk. Rwakatare, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), alisema watoto hao walidondoka wakati waumini wa kanisa hilo walipokuwa wakiomba na kumtukuza Mungu.
Mchungaji huyo, alikaririwa na vyombo vya habari akisema watoto hao walianguka kutoka juu katika eneo la kanisa hilo baada ya nguvu za giza kushindwa kutokana na maombi ya kawaida yaliyokuwa yakiendelea ndani ya kanisa lake.
Hata hivyo, siku kadhaa baada ya mkutano na waandishi wa habari, Mchungaji Dk. Rwakatare, alionekana tena kwenye luninga akiwa katika shughuli za kiroho na kuwahoji watoto hao waliodaiwa kudondoka kanisani hapo, waliosema walikuwa wakitokea Mwanza wakielekea Mtwara.
Akiwa na wachungaji wengine wa kanisa hilo, Dk. Rwakatare, aliwaombea watoto hao na kuwaeleza waumini wake kuwa, hayo ni matunda ya maombi yao na kwamba ‘Yesu wa kanisa lao’ anatenda miujiza.
Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na taarifa za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na masuala ya kishirikina kudondoka kutoka angani kila mara wanapopita katika anga za baadhi ya makanisa nchini.
Hata hivyo, matukio hayo ambayo yamekuwa yakiripotiwa makanisani na katika vyombo kadhaa vya habari, yamekuwa yakiibua maswali mbalimbali kuhusu uthabiti wake ambao ni vigumu kutolewa maelezo katika hali ya kawaida.
Kutoka: Tanzania Daima

Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
hii inadhihirisha tu jinsi ambavyo hawa wachungaji wetu, wengi wao ni fix-kamba tu...otherwise huyu mama angekua serious na nguvu za roho mtakatifu, angeweza kutambua hilo mapema...sometimes GOD exposes the other side of a person thru simple acts...after all,siasa na dini wapi na wapi?
na mdau, dsm, - 29.03.08 @ 10:20 | #3962
Acheni kuwatapeli watu kwa kisingizio cha kuwa na uwezo wa kiungu. Hii tabia inayofanywa na baadhi ya makanisa na wachingaji wao eti wananguvu ya kiungu ni uhuni na utapeli na inakera sana. Watoto hawa wasilaumiwe, bali wanaowatumia kwa maslahi yao binafsi ndo wa kulaumiwa. Siamini watoto wadogo kama hawa wakabuni mkakati huu wanaodaiwa kuuendesha, lazima viongozi wa makanisa wanaojifanya wananguvu ya uungu wanawatumia kujitangazia umaarufu na kujipatia wafuasi. Yakowapi sasa.
na Kely - 29.03.08 @ 10:21 | #3963
nakubaliana nawe mdau. Mungu hamfichi mnafiki.
na Kely - 29.03.08 @ 10:24 | #3965
Ama kweli duniani kuna mambo! yaani Mchungaji, Dr. Rwakatare na waumini wote wa Kanisa la Mikocheni wameingizwa mkenge na hao watoto?
Watoto Yusufu na Ramadhani inabidi watafutiwe Chuo wasome ili waendeleze vipaji vyao vya usanii, Taifa lisiache tu vipaji kama hivyo vikapotea bure!
na A.S. Mbweni, DSM, - 29.03.08 @ 10:26 | #3967
Huu mama ni mbunge.Hivi kweli tunakuwa na wabunge wapumbavu namna hii. Sasa huko bungeni ataenda kusema nini kama anaweza kuwa na akili ndogo kiasi cha kutapeliwa na watoto. Linalo nitia uchungu ni kwamba anaweza kuwadanganya waumini wake kwamba ana nguvu za kiroho wakati anajua fika kwamba hamna lolote. Huu ni ufisadi, tena ufisadi mkubwa sana. Hawa wachungaji wanaojitia wana nguvu za kiroho ni mafisadi wakubwa. Kazi yao ni kutapeli tu watu dhaifu wasiokuwa na muono wa maisha. Hawa ni wakufilisiwa tu hamna jingine.
na chombeza, bongo, - 29.03.08 @ 10:41 | #3971
Acha usanii wewe mama lwakatare na kwa nini kanisa lako una liita mikocheni b assemblies of God instead of TANZANIA assembies of God.
Kwa nini hujatumie kile kitambaa chako kuwajua watoto hao kwa kipindi chote ulichokuwa unatangaza kudondoka kwa watoto hao na ukawaita misukule????????????
na P.K.Mduma, Dar, - 29.03.08 @ 10:44 | #3973
1 comment:
safi
Post a Comment