Monday, April 21, 2008


Ditopile Ukiwaona Mzuzuri "Brother Dito" pichani, amefariki alfajiri ya Aprili 20 2008 katika Hoteli ya Hillux mjini Morogoro. Marehemu alikuwa na mkewe mdogo katika shughuli za kifamilia. Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Marehemu Upanga jijini Dar es Salaam.

Marehemu Ditopile anataraji kuzikwa Aprili 22 2008 katika makaburi ya familia yaliyopo Segerea mara baada ya swala ya atdhuhuri.

Marehemu Ditopile ameacha wajane wawili na watoto watatu.

KWANIABA YA WADAU WOTE WA BLOG HII NATOA POLE KWA WAFIWA NA KUMUOMBEA MAREHEMU ALAZWE MAHALA PANAPOMSTAHILI AMINA.

Mwenyezi Mungu Amlaze Pema, Amin!


No comments: