Sunday, April 13, 2008

Mkataba wa TICTD

uliokiuka utaratibu




• Ni kaluli Mkaguzi mkuu wa Serikali
• ‘Madudu’ kumkem ya matumizi yabainika mashirika ya umma

MKAGUZI na mdhabiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludavick Utouh, amesema kuwa mkataba wa kuiongezea muda kampuni ya kuhudumia Makontena katika bandari ya Dar es Salaam (ITCTS) ulitiwa saini kinyume na manunuzi ya umma.

Akizungumza mjini hapa wakati akiwasilisha ripoti ya ukaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2007, alisema utaratibu ulotumika ulikiuka sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2004.

MKATABA WA TICTS ULIOKIUKA UTARATIBUAlisema, ofisi yake imebaini upungufu huo wakati ikipitia taarifa za hesabu za Mamlaka ya bandari (THA), ambapo hakuona sababu za kuongeza miaka 25, wakati 10 haijamalizika.

Awali, muda wa mkataba huo ulikuwa miaka 10, ambapo kampuni hiyo iliongezwa mingine 15 na hivyo kuifanya iwe 25. mkataba huo umezua malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali, wakiwemo wabunge.

Mkaguzi huyo alisema ofisi yake imetoa mapendekezo kadhaa serikalini kuhusu mkataba huo.

Kwa upande mwingine, utouh alisema ukaguzi maalumu ulifanywa katika akaunti ya malipo ya Nje (EPA) ya Benki kuu (BOT), alibaini kuwa kiasi cha sh, bilioni 133 zililipwa, ambapo sh. Bilioni 90 zimethibitishwa kuwa zilitolewa kinyume cha utaratibu.
Mbali ya utata huo, pia kiasi kingine cha sh. Bilioni 42 zinahitaji kuchunguza zaidi kujua ni jinsi gani zilitolewa au kutumika.

Kutokana na uchunguzi mwingine unaoendeshwa na kamati iliyoteuliwa na rais Jakaya Kikwete, ACG alisema ofisi yake imesimamishwa kwa muda uchunguzi na kwamba utaendelea baada ya kumalizika kwa kazi ya kamati hiyo.

Akizungumzia mashirika mengine alisema Shirika la Hifdhi ya Taifa (TANAPA), lilifanya malipo ya awali bila kuwa na dhamana kabla ya kupokea mali na vifaa vyenye tathmini ya sh. Bilioni 1.9.

Kutokana na kukiuka utaratibu huo, amelishauri kufuata taratibu za kisheria pale litakapo taka kufanya manunuzi mengine ili lisiliingize taifa kwenye matatizo.

Kama ilivyo TANEAPA, Bodi ya Tumbaku pia inatunukiwa kununua bidhaa na huduma mbalimbali zenye thamani ya sh,223,694 bila kufuata sheria.

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pia alisema kuwa mashirika ya umma na taasisi 91 za serikali zilikaguliwa, ambapo 80 kati ya hizo zilipata hati za kuridhisha, wakati 10 zilipata hati zenye mashaka na shirika moja lilikabidhiwa hati chafu.

Mashirika na taasisi hizo ni pamoja na Mamlaka za Maji 19, Bodi za Usimamizi 19, Vyuo vya Elimu ya juu 15, Mashirika ya Umma 15 na Taasisi 15.

Aidha, katika kipindi hicho, shirika la Posta, Stamico, Bodi ya Biashara za Nje (BET) na Taasisi moja ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) hayakuwasilisha kwa wakala husika makato ya kisheria yanayofikia sh 29,333,119,002.

Alisema hali hiyo isipodhibitiwa, inaweza kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyakazi waliohusika wakati wa kudai mafao yao mara watakapostaafu, na kwamba mashirika hayo yanaweza kutozwa faini kubwa na mashirika au taasisi husika na hivyo kuingiza serikali kwenye madeni yanayoepukika.

Ofisi hiyo imebaini kuwa shirika la Mfuko wa Hifadhi za Jamii (NSSF) na lile la Posta, yalizembea kufuatilia madeni kutoka kwa watu na taasisi zilizokopa.

CAG alisema kuwa, NSSF walishindwa kukusanya madeni ya zaidi ya sh. Bilioni nne wakati Posta wateja mbalimbali hawakulipa sh. 196,973,814.

Kwa upande mwingine, shirika la Umeme nchini (TANESCO) lilishindwa kudai zaidi ya sh. Biloni mbili kutoka kwa kampuni ya Dowans Holdings, zilizotokana na ukiukwaji wa makubaliano ya mkataba kati ya pande hizo.

Iwapo zingepatikana, fesha hizo zingelisaidia kukabiliana na hali ngumu inayolikabili pamoja na majukumu liliyonayo.

Hali ni hiyo pia kwa mashirika ya Posta na Tanzania Standard Bewspapers yaliyolipa kimakosa zaidi ya sh. Milioni 300 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya Hesabu za Serikali, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Hesabu za Serikali, John Cheyo, alisema ubadhirifu ulipojitokeza na kuwabana wahusika.

“Tunawapongeza sana kwa kuleta ripoti kwa wakari, pia ni vizuri mmewakumbuka wastaafu maana wanaweza kuanza kujisaidia kabla ya wakati, lakini pia endelea kufanya kazi bila wote,” alisema.

Naye mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya mashirika ya Umma, Zitto Kabwe alisisitiza watafuatilia ili Ofisi ya Ukaguzi na Udhibiti wa Hesabu ijitegemee ili iweze kufanya kazi zake kwa uhuru.

“Lakini pia inabidi ufanye ukaguzi BoT maana ripoti itakuwa yako na haitahusiana na ile ya kamati (ya
Rais), mimi pia naomba mnipe mashirika ambayo hayapeleki michango ya malipo ya wastaafu ili nianze nayo katika kamati yengu,” aliongea.

(Imetolewa na Uhuru Issue no 19909, 12/4/2008)

No comments: