Tuesday, April 29, 2008


Mtoto aliyekatwa kichwa

Kuzikwa Leo..


Pichani Ramadhani Mussa (12)ambae anashikiliwa na polisi Mkoa wa Ilala kwa kukutwa na kichwa cha mtoto mdogo Salome Yohana (3) alichokuwa amekibeba katika mfuko wa rambo kwenye hospital ya tIafa ya muhimbili Hivi karibuni.Kwa sasa bado anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi..
------------------------------------------------------------

MTOTO Solome Majana (3) aliyefariki wiki iliyopita katika mazingira ya kutatanisha baada ya kichwa chake kutenganishwa na kiwiliwili chake anazikwa leo makaburi ya Tabata. Akizungumza na majira jana baba wa mtoto huyo, Bw. Yohana Majana (26),alisema wamekamilisha taratibu zote za kipolisi na waliruhusiwa kuchukua mwili huo wakati wowote kuanzia jana asubuhi.

"Tumemaliza taratibu zote za polisi na leo (jana asubuhi) tulikubaliana kuwa muda wowote tukiwa tayari tuuchukue mwili wa marehemu kwa maziko, tumeruhusiwa kufanya hivyo."alisema Akizungumzia mkasa huo alisema serikali inatakiwa kuamini kuwa uchawi upo na watu wanaobainika kuhusika katika matukio ya kichawi kama lililomtokea kwa mwanae Salome, wawajibishwe.

Bw. Majana, alisema yapo matukio mengi ambayo yanatokea ambayo yanahusika na masuala ya uchawi lakini kutokana na Serikali kutotilia mambo yamekuwa yakienda hivi hivi na watu wengi kuathirika. Alisema mtoto wao Salome alitoweka nyumbani Aprili 25 mwaka huu jioni na kesho yake walikuta mwili wake ukiwa umekatwa kichwa.Habari hii na Eben-Ezery Mende



No comments: