
Rostam Aziz :
Richmond 'No coment'
Na Said Mwishehe
Gazeti la Majira
MBUNBGE wa Igunga Bw.Rostam Aziz, CCM ambaye alipigwa 'stop'kuwasilisha hoja yake bungeni kuhusu sakata la mkataba wa kampuni hewa ya kuzalisha umeme ya Richmond amesema hana cha kuzungumza kuhusu hatua hiyo ya Bunge.
Akizungumza kwa njia ya simu na Majira jana jioni, Bw.Aziz alisema kwa hana la kuzungumza kuhusu suala hilo ambalo lilisubiriwa kwa hamu na wananchi wengi.
Kusimamishwa kwa hoja hiyo kulizua malumbano kati ya Naibu Spika wa Bunge aliyekuwa akiendesha kikao hicho na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), aliyedai Bi Makinda anazuia hoja kwa lengo la kulinda maslahi ya Chama chake CCM.
Majira ilitaka kujua nini msimamo wa Bw.Azizi baada ya hoja yake kuzuiwa bungeni na kama ana mpango wa kuchukua hatua zozote kuhakikisha ujumbe aliokuwa nao ndani ya hoja yake anautoa.
"Nasema sina 'coment,' naomba ieleweke kuwa sina coment kwa sasa"alijibu Bw.Aziz na kisha akakata simu.
Katika kikao cha Bunge cha juzi mjini Dodoma, Bw.Aziz alitarajiwa kuwasilisha hoja yake kuhusu sakala la Richmond matokeo yake alikatazwa kuiwakilisha kutokana na taratibu za Bunge na kuleta kizazaa hicho.
Bibi Makinda wakati akisoma ufafanuzi huo muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha Bunge juzi, alisema hoja binafsi inatakiwa kupita kwenye kamati za chama husika cha siasa, kabla ya kuwasilishwa kwa Katibu wa Bunge ili iweze kujadiliwa.
Naibu Spika huyo alisema ili kuvitendea haki vyama vya siasa bungeni kanuni 110 imewekwa mahususi kwa ajili ya kuviwezesha vyama vyenywe vijiwekee utaratibu bora wa kuratibu masuala ya vyama vyao,ikiwa ni pamoja na uratibu wa kushughulikia masuala mbalimbali yanayokusidiwa bungeni, ili kuweka uwajibikaji wa pamoja wa kichama bungeni.
No comments:
Post a Comment