
Wamlazimisha msichana
kufanya mapenzi na mbwa
WATU wawili wanashikiliwa na Polisi wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za kumlazimisha msichana mwenye umri wa miaka 11 kufanya mapenzi na mbwa, na kulipwa ujira wa Sh 1,000, imefahamika.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Sengerema, Rashid Seif alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Machi 21, mwaka huu, saa tatu usiku katika kambi ya utafiti wa madini ya Nyanzaga inayomilikiwa na Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick Tanzania.
Seif alisema msichana huyo ambaye jina lake linahifadhiwa, anasoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Sota iliyopo Kijiji cha Ngoma Kata ya Igalula, na alikwenda kwenye kambi hiyo kwa kuchukuliwa na rafiki yake kwa lengo la kwenda kutembea katika kambi hiyo.
Alisema msichana huyo alirubuniwa kwenda huko na msichana aliyetambuliwa kuwa Shija Madata, na ilipofika majira ya saa tatu usiku, binti huyo alipelekwa katika banda la mbwa; ambako inadaiwa alivuliwa nguo kwa nguvu na kuanza kufanya mapenzi na mbwa huyo chini ya wahudumu wa kambi hiyo.
OCD aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Jobu Mlama (30) ambaye ni sungusungu wa Kijiji cha Sota na anayefanya kazi ya upishi katika kambi hiyo na Aniseti Ndege (30), mwajiriwa wa Barrick kama mtunza mbwa huyo. Wote wanadaiwa kushirikiana na Shija kufanikisha mbwa kumuingilia mwanafunzi huyo.
Inadaiwa kuwa Shija alimrubuni mwanafunzi huyo kufanya mapenzi na mbwa huyo baada ya vijana hao walinzi kumpa Sh 70,000 kama ujira wa kazi hiyo, ambaye naye alimlipa binti huyo Sh 1,000 baada ya kumaliza kufanya mapenzi na mbwa huyo kwa muda wa saa moja.
Mkuu huyo wa Polisi wa Wilaya alisema Shija alitoroka baada ya kusikia taarifa za kutafutwa na polisi, na anatafutwa ili kujibu shitaka linalomkabili. Naye Ofisa Uhusiano wa Barrick Tanzania, Teweli Teweli, alisema kampuni hiyo inaalani kitendo kilichofanywa na mwajiri wao, Ndege kwa sababu siyo tabia ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na kimekosa utu na siyo cha busara.
Alikiri kuwa Ndege ameajiriwa kama mlinzi katika kambi hiyo, na kwamba siku ya tukio, inaaminika mpenzi wake, Shija alikwenda hapo na binti huyo anayedaiwa kuingiliwa na mbwa; wakapika na kula kabla ya kutokea kwa tukio hilo la aina yake.
No comments:
Post a Comment