Ana kwa ana na
Miriam Chemoss

Endapo kuchanganya utaifa,damu na tamaduni mbalimbali ni mojawapo ya chachu za mafanikio fulani hapa duniani, basi ushahidi wa dhana hiyo unaweza kuupata kwa kuangalia maisha ya mrembo Miriam Chemmoss(pichani).
Miriam ni muigizaji, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na pia mwanamitindo (model) ambaye mpaka hivi leo ana haki ya kusimama na kujivunia rekodi yake katika ulimwengu changamani wa sanaa na maonyesho. Mwenyewe anasema safari yake ndio kwanza inaanza kwani bado ana ndoto na malengo chungu mbovu ya kutimiza.Hivi leo kazi zake nyingi anazifanyia kutokea jijini New York nchini Marekani anapoishi.
Kama ilivyo kwa wasanii wengi, safari ya Miriam katika ulimwengu wa sanaa inaanzia tangu akiwa mwanafunzi mdogo. Lakini ni pale alipohamia jijini New York mwaka 2004 na kujiunga na kundi maarufu lililojulikana kama The Marvallettes Revue lililokuwa chini ya Pam Darden, ndipo nyota yake ilipoanza kung’ara ipasavyo. Baadaye alijiunga na kundi lingine maarufu la Soukouss Stars kama mwimbaji pekee wa kike na mnenguaji kabla ya kuamua kuimba peke yake(solo artist) mwaka 2006.
Kwa upande wa uigizaji, Miriam ameshaigiza katika show mbalimbali maarufu ikiwemo ile ya “District” katika kituo maarufu cha televisheni cha CBS.Pia ameshiriki katika “Bedford Diaries” ya Warner Bros.Sauti yake imetumika katika matangazo mbalimbali ya biashara kama vile Western Union(USA-African Market) nk.Kwa upande wa mavazi Miriam amewahi kuwa model wa jeans za Levi’s, Getty Images/Brazilian Salsa Club(Print),Bebe Noir Clothing Line,New York nk.Mwaka 2007 mtandao wa http://www.jamati.com ulimtaja Miriam katika orodha yao ya Top 10 Sexiest African Women akiwa ni miongoni mwa wasichana wawili kutoka eneo la Afrika Mashariki.
Hivi karibuni BC ilipata fursa ya kufanya mahojiano rasmi na Miriam. Katika mahojiano haya, Miriam anaweka wazi kuhusu utaifa wake. Je Miriam ni Mtanzania au Mkenya? Nini maoni yake kuhusu sanaa ya filamu nchini Tanzania? Anatoa ushauri gani kwa wadau wa sanaa hiyo? Na je,kwa msiomfahamu, Miriam ni nani? Ana malengo gani? Kwa hayo na mengineyo mengi, fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
Toka Bongo Celebrity
No comments:
Post a Comment