Thursday, May 29, 2008

Azaa mtoto wa ajabu


Na Catherine Kassally.


Binti aliyefahamika kwa jina la Foibe Shedrack Kusaga (22), mkazi wa kijiji cha Igando Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, amejifungua mtoto wa ajabu ambaye hana mkono wala miguu...


Foibe ambaye alifika katika ofisi zetu akiwa ameambatana na ndugu yake alisema kuwa, alijifungua mtoto huyo wa kiume aliyempa jina la Bahati Shedrack miezi minne iliyopita lakini kwa bahati mbaya hakikuwa kiumbe kilichokamilika.

Aidha, msichana huyo aliongeza kuwa, baada ya kujifungua alimpatia taarifa mzazi mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Andrew ambapo alipofika hospitalini na kukiona kiumbe hicho, alikana kuwa sio chake.

“Niliumia sana kwani nilipomfahamisha mzazi mwenzagu juu ya kujifungua kwangu kiumbe hicho, alikataa kuwa sio mwanaye huku akinituhumu kuwa nilifanya mapenzi na mtu mwingine. Kuanzia siku hiyo sikumuona tena, nimebaki nikipata tabu peke yangu,” alisema binti huyo kwa masikitiko .

Hata hivyo, kutokana na ugumu wa maisha aliokuwa akiupata mkoani Dodoma, Foibe alilazimika kuja jijini Dar es Salaam ambapo kwasasa anaishi na baba yake mdogo aitwaye Musa Kusaja maeneo ya Manzese Midizini.

Bahati ambaye kwasasa ana miezi minne, anaishi maisha ya tabu sana hivyo mchango wako huenda ukamuokoa. Kama umeguswa na una nia ya kutaka kumsaidia, wasiliana nasi kwa simu namba- 0773 744 799 au 0713-070116.

Kutoka Global Publishers (Tanzania)



No comments: