Monday, May 26, 2008

Kifo cha Ballali:

Serikali inaficha ukweli

Wanasheria


BAADHI ya wanasheria wameshangazwa na usiri wa serikali kuhusu kuugua hadi kufa kwa aliyekuwa Gavana wa Benki ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Ballali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima Jumapili mwishoni mwa wiki, wanasheria hao walisema lazima serikali inaficha jambo kuhusu Dk. Ballali.

Mmoja wa wanasheria hao, Mabere Marando, alitoa lawama kuhusu ukimya wa serikali, katika kuugua hadi kufariki dunia kwa Dk. Ballali, na kuongeza kwamba kutawafaidisha watuhumiwa wa wizi wa fedha katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA), uliofanyika BoT.

“Nimesikitishwa sana na kifo cha Dk. Ballali, alikuwa Mtanzania mwenzetu. Lakini kinachosikitisha zaidi ni ukweli kwamba kifo chake kitaathiri sana uchunguzi wa wizi wa fedha za EPA.

“Ukimya wa serikali kuhusu kuugua hadi kufa kwa Dk. Ballali, unashangaza, ni wazi kuwa kuna jambo inaficha, kwa sababu haiwezekani isijue mahali alipo gavana wake wakati ilikuwa ikimlipia sehemu ya gharama za matibabu kama tulivyoelezwa na gavana wa sasa,” alisema Marando.


Bofya na endelea kusoma....



No comments: