Kikwete awapatanisha
Museveni, Kabila
Evance Ng’ingo
Daily News; Monday, May 12, 2008
RAIS Jakaya Kikwete amefanikiwa kuwapatanisha marais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Yoweri Museveni wa Uganda ambao sasa wanaangalia uwezekano wa kufungua ofisi za ubalozi katika nchi zao.
Marais hao wawili waliwasili nchini jana asubuhi kwa ziara ya siku moja ya kikazi kufuatia mwaliko wa Rais Kikwete na wakatumia fursa hiyo kujadili hali tete ya uhusiano baina yao na masuala ya usalama na uchumi.
Rais Kikwete ndiye aliyeanzisha mchakato wa mazungumzo hayo ya amani kwa kuwakutanisha marais hao kwa mara ya kwanza huko Ngurdoto, Arusha, mwaka jana, wakati huo uhusiano kati ya Uganda na DRC ulikuwa usababishe nchi hizo mbili zipigane vita.
Taarifa iliyotolewa mwishoni mwa kikao hicho kilichofanyika Ikulu na kusomwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ilisema katika suala la usalama Kabila na Museveni walikubaliana kuondoa uhasama wa kijeshi katika mpaka baina yao.
Ilisema viongozi hao ambao waliondoka kurudi kwao baadaye jioni, walimsisitiza kiongozi wa uasi wa kikundi kinachopingana na Serikali ya Uganda cha Lord’s Resistance Army (LRA) Joseph Kony, kufuata makubaliano ya Juba yanayomtaka kuacha kuendeleza vita.
Kuhusu ushirikiano katika sekta ya uchumi wakuu hao walieleza kuridhishwa na ushirikiano uliopo ikiwamo haja ya kusainiwa mikataba ya maendeleo baina ya mawaziri wa madini, nishati na umeme.
Pia walikubaliana kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuomba misaada ya fedha kutoka Jumuiya ya Ulaya na mashirika mengine kufadhili mradi wa umeme kati ya Uganda Magharibi na kaskazini mashariki mwa DRC.
Baada ya mazungumzo hayo ya jana, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais wa Uganda anayeshughulikia Mambo ya Nje, Isaac Msumba na mwenzake wa DRC Mbusa Nyamisi walisaini mikataba ya makubaliano.
Akizungumza baadaye, Waziri wa Ulinzi wa DRC Chikez Diemu alisema kuwa jeshi la nchi hiyo litalazimika kutumia nguvu kuwaondoa raia wa Uganda ambao watakaidi kurudi nchini kwao kutoka Kongo kwa hiyari.
Diemu alisema kuwa nchi hizo mbili zinatakiwa kuacha mapambano na kuanza upya kujenga nchi zao katika uchumi kuweza kuleta maendeleo.
Mkutano huo ulichukua takribani saa nne huku ambako kila upande ulionyesha kuridhishwa na makubaliano hayo.

No comments:
Post a Comment