Tuesday, May 20, 2008

MPASUKO WA KISIASA ZANZIBAR

Balozi wa Ujerumani

airushia kombora CCM



na Kulwa Karedia

BALOZI wa Ujerumani nchini, Wolfgang Ringe, amesema mgawanyiko mkubwa uliomo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umesababisha kukwama kwa mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar kati ya chama hicho na mahasimu wao kisiasa, Chama cha Wananchi (CUF).

Aliyasema hayo jana muda mfupi baada ya uzinduzi wa kitabu cha ‘Maendeleo Dialogue na miaka 15 tangu kuingia mfumo wa vyama vingi Tanzania’, kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam.

“Mazungumzo haya tumekuwa tukiyafuatilia kwa karibu mno, lakini kumeonekana mgawanyiko ndani ya CCM, kwani imeonekana kuna CCM Zanzibar na CCM Tanzania Bara, hali inayoonekana kuwa kikwazo cha kufanikisha mazungumzo haya,” alisema Balozi Ringe.

Bofya na endelea kusoma.....



No comments: