Zanzibar yamtikisa
Kikwete
na Mwandishi Wetu
KUPANDA kwa kasi kwa joto la kisiasa katika Kisiwa cha Pemba, kunaonekana kuwa ni dalili za mwanzo za kutikisika kwa Rais Jakaya Kikwete, na pengine kukwama kwa ‘ndoto’ yake ya miaka miwili iliyopita ya kuweka historia ya kupatikana kwa ufumbuzi wa kile alichokiita Mpasuko wa Kisiasa Zanzibar.
Matukio ya hivi karibuni, yamechochewa na uamuzi wa vikao viwili vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukataa mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya pamoja ya muafaka iliyokishirikisha chama hicho tawala na mahasimu wake wakubwa wa siasa za Zanzibar, Chama cha Wananchi (CUF).
Tukio la kwanza lililoonekana kumgusa moja kwa moja Rais Kikwete ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, ni lile la wazee 12 wa kutoka Pemba, iliko ngome kuu ya kisiasa ya CUF, kuandamana hadi katika Ofisi za Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) zaidi ya wiki moja iliyopita.
Bofya na endelea kusoma......
No comments:
Post a Comment