Zanzibar:
Uhafidhina Visasi na
Miafaka Isiyodumu (1)
na Joseph Mihangwa
TAFSIRI ya neno “Zanzibar” ni “Zenj”na “bar”. Zenj maana yake ni “nyeusi”na “bar”inamaanisha nchi. Kwa hiyo, “Zanzibar” ni “nchi nyeusi”au nchi ya Weusi.
Zanzibar inaundwa na visiwa vikuu viwili; Unguja (Kilomita mraba 1,464)na Pemba (Kilomita mraba 868). Zanzibar ina mengi ya kujitofautisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki; Zanzibar ndiyo mzalishaji mkubwa wa zao la karafuu duniani na ilikuwa nchi ya kwanza kusini mwa jangwa la Sahara kuendesha uchaguzi chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1957.
Lakini kubwa kuliko yote ni kwamba Zanzibar ni nchi ya kihafidhina,na migogoro ya kisiasa isiyoisha kwa karne tatu mfululizo,kuanzia karne ya 19 hadi sasa , visasi na miafaka isiyodumu.
Ukorofi wa kisiwa hiki na athari zake kwa ukanda wa Afrika Mashariki unathibitishwa na usemi wa karne ya 19 kwamba: “Zanzibar wanapopiga chafya, bara yote huugua mafua”.

No comments:
Post a Comment