Serikali yafichua
Kigogo wa Dowans
- Ni Mtanzania, kiongozi wa CCM
- Hoseah kung’olewa TAKUKURU
- Akina Karamagi wachunguzwa
MAKAMPUNI ya kuzalisha umeme ya Richmond na Dowans yanamilikiwa na mtu mmoja, MwanaHALISI limegundua.
Vyanzo mbalimbali vya taarifa ndani ya serikali vimekiri pia kwamba hayo ni makampuni ya mfanyabiashara mmoja mashuhuri raia wa Tanzania.
Kupatikana kwa taarifa hizo kumefuta madai ya baadhi ya viongozi nchini waliokuwa wakisema kuwa Dowans ni kampuni iliyosajiliwa nchini Costa Rica, Marekani Kusini.
Lakini taarifa zinasema kuwa serikali imethibitishiwa na Mwanasheria Mkuu wa Costa Rica kwamba nchini humo hakuna kampuni inayofahamika kwa jina la Dowans.
Aidha, imefahamika kuwa akaunti za kampuni ya Dowans, ambayo mfanyabiashara Rostam Aziz amewahi kukiri kufahamiana kibiashara na maofisa wake, ziko Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu.
Bofya na soma zaidi kwenye gazeti la MwanaHALISI.
No comments:
Post a Comment