Friday, May 16, 2008


Kanisa la wanawake

wajane kusali

uchi laanzishwa



*Wasema si tatizo kwani mtoto huzaliwa bila nguo

Na Samwel Mwanga, Maswa

KANISA la ajabu limeibuka wilayani Maswa mkoani Shinyanga, likiwa na waumini wanaoendesha ibada wakiwa uchi na baadhi yao wakiwa ni wanawake wajane na ambao ndoa zao zimevunjika kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana wilayani hapa na kuthibitishwa na baadhi ya wanawake wanaofanya ibada katika Kanisa hilo limeelezwa kuwa waumini wake ni waliookoka, ibada zake zinaendeshwa katika moja ya madarasa ya shule ya Msingi Binza.

Kanisa hilo linadaiwa kuongozwa na Mchungaji aliyejulikana kwa jina moja la Claud ambaye inasemekana ametokea Kahama mkoani hapa.

Bofya hapa na usome zaidi:

No comments: