Vitambulisho vya uraia,
ufisadi unaopikwa
MRADI mkubwa wa Vitambulisho vya Taifa bado umegubikwa na utata, huku kukiwa na sura dhahiri ya ukosefu wa uwazi na hata kuonekana ni kinyang’anyiro cha ulaji.
Wakati Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, akitangaza kuwa zabuni ya mradi huo itatangazwa kabla ya mwisho wa wiki hii, tayari ofisi ya mradi huo ipo na inafanya kazi na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) ameteuliwa.
Masha anasema: “Ninachofahamu mimi ni kwamba tutatangaza tenda kabla ya mwisho wa wiki. Tutatangaza kwa uwazi kabisa.”
Raia Mwema ilipowasiliana na maofisa wa Idara ya Uhamiaji, iliambiwa tayari ofisi ya mradi huo ipo Kinondoni, Dar es Salaam, na CEO wake anaitwa Dicksom Maimu.
No comments:
Post a Comment