Friday, May 16, 2008

Wapemba si

wahaini



Na Simon Mhina

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani hatua ya Serikali kuwashikilia watu waliowasilisha waraka Umoja wa Mataifa wakitaka kisiwa cha Pemba kijitenge na kuwa huru.

Aidha kituo hicho kimesema kuwasilishwa kwa waraka huo UN sio uhaini kwa kuwa ni suala la maoni linakubalika kikatiba.

Akizungumza na Nipashe ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, mwanasheria wa kituo hicho, Bw. Clarence Kipobota, alisema kitendo cha watu hao kutoka Pemba kuandika waraka na kutoa madai hayo, hakikidhi haja ya wananchi hao kushtakiwa kwa kosa la uhaini.

Alisema hata hatua ya Serikali kuwashikilia watu hao kwa muda mrefu na kuwahifadhi sehemu isiyofahamika, huku ikiwakataza ndugu zao kuwaona, ni ushahidi mwingine kwamba imekosa vifungu vya sheria vya kuwashtaki.

Akifafanua, mwanasheria huyo alisema kwa mujibu wa Kanuni za Makosa ya Jinai, lazima ithibitike kuwepo na kunuia uovu pamoja na kitendo kiovu

``Mambo hayo yakithibitika ndipo kunazaliwa neo jinai`` alisema Bw. Kipobota.


Bofya hapa usome zaidi

No comments: