Sunday, June 01, 2008

Askofu Mokiwa ang’aka

nchi imepoteza mwelekeo



na Rahel Chizoza, Dodoma

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa, amesema uchumi wa nchi umeporomoka licha ya taarifa za kuimarika kwa hali hiyo kwa asilimia kadhaa.

Akifafanua kauli yake kuhusu hali ya uchumi, alisema maisha ya Watanzania wengi hali zao ni duni, na zimeendelea kuwa hivyo siku hadi siku kwamba umefika wakati jamii inakosa matumaini ya kuishi.

“Watu wenye maisha mazuri hapa Tanzania ni wachache, wengi wao maisha yao ni duni sana, ni vema viongozi wawasaidie wananchi kuondokana na hali hiyo angalau kwa kudhibiti mfumuko wa bei,” alisema askofu huyo katika mazungumzo yake na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana.


Bofya na endelea...


No comments: