Saturday, June 07, 2008

Heri ‘Mzee Abdallah’ wa

Bagamoyo ya zama zile



Johnson Mbwambo

NAAMINI wengi wetu tumepata kuisikia simulizi ya kale inayomhusu Mzee Abdallah wa Bagamoyo - simulizi iliyotumiwa na Wazungu kukejeli fikra, visheni na mitazamo ya Waafrika wajasiriamali wa zama za ukoloni.

Mzee Abdallah alikuwa ni tajiri mkubwa kwa kiwango cha Bagamoyo cha enzi hizo. Bagamoyo nzima alikuwa ndiye pekee mwenye nyumba ya bati na boti ya uvuvi.

Kwa wakazi wa Bagamoyo wa zama hizo, ukizungumzia kitu chochote kizuri unamzungumzia Mzee Abdallah. Ukisifu chakula kizuri ulichokula, utaulizwa: Kinafanana na anachokula Mzee Abdallah? Ukiisifu nguo nzuri uliyonunua utaulizwa: Inafanana na anayovaa Mzee Abdallah? Ilimradi kila kitu kizuri ni Mzee Abdalah …Mzee Abdallah… Mzee Abdallah.


Bofya na endelea>>>>>



No comments: