Saturday, June 07, 2008

AYA ZA AYAH

Wakivimbiwa wanatishiwa

na uvimbe



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi Frank,

HAYA bwana, wewe unigeuzie kibao tu. Eti kazi yangu kumwongelea bosi na mambo zake tu! Eti unathubutu kuniuliza nina mahusiano gani naye? We Frank huoni hata haya kuniuliza maswali kama hayo?

Kama umechoka kusikia stori zangu si useme tu. Mi Hidaya wako nakaa ndani ya nyumba tangu asubuhi hadi usiku, sana sana napelekwa sokoni kwa gari na kurudi kwa gari, nitakupaje michapo ya mitaani. Eti kwa kuwa lishangingi lako lilinitisha, na lilinitisha kweli, wewe unatafuta kujitetea kwa kuleta hadithi za Alinacha?


Bofya na endelea>>>>>

No comments: