Tuesday, June 03, 2008

Prof. Haroub Othman:

Kikwete aongoze

mazungumzo mwenyewe



na Prisca Nsemwa

PROFESA Haroub Othman, wa Taasisi ya Taaluma za Maendeleo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), amemtaka Rais Jakaya Kikwete, kuchukua mamlaka kamili ya kuongoza mazungumzo ya muafaka wa Zanzibar, badala ya kuwaachia Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad, na mwenzake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, ili kuleta suluhu na kulinda muungano.

Mbali na hilo, profesa huyo mtaalamu wa masuala ya siasa, alisema kuwa Kikwete ndiye rais wa muungano, hivyo jukumu ambalo anatakiwa kulifanya kwa haraka iwezekanavyo ni kuendesha mazungumzo hayo yeye mwenyewe, ili kuepuka madhara makubwa ambayo yanaweza kutokea kwa taifa.


Bofya na endelea>>>>>



No comments: