Wednesday, June 04, 2008

Rais wa Gambia

atishia kuwakata vichwa

mashoga, wasagaji


"The Gambia is a country of believers... sinful and immoral practices [such] as homosexuality will not be tolerated in this country",
Yahya Jammeh


Rais wa Gambia, Alhaj Yahya Abdul-Aziz Jemus Junkung Jammeh ametishia kuwakata vichwa mashoga na wasagaji watalii watakaoingia nchini Gambia. Kufuatia habari zilizoandikwa kwenye gazeti la Aftenposten, kuwa Rais Jammeh anakusudia kutunga sheria kali zitakazowahusu mashoga na wasagaji.

Jana mtalii mmoja wa Kihispania amekamatwa kwa kumjaribu dereva wa taxi mjini Banjul. Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Norway, Bw. Thor- Henrik Andersen, amesema kuwa Norway inafuatilia kwa makini suala hilo na mashoga na wasagaji wa Norway wameonywa kuwa waangalifu watakapokuwa nchini Gambia.


Mengi juu ya hilo, bofya hapa na endelea kwenye makala za BBC News zilizopita.



No comments: