Wednesday, June 04, 2008

Mgomo wa wa waalimu,

wafanyakazi wa serikali

umekwisha!


Picha toka Dagbaldet.


Makubaliano yamefikiwa leo saa 5 asubuhi kati ya wafanyakazi wa taaluma mbalimbali wa manispaa za Norway (Confederation of Unions for Professionals - Unio) na waajiri wao, Manispaa za Norway (Public Sector Emploers Group KS). Wafanyakazi 11200 wa manispaa za Norway walikuwa kwenye mgomo ulioanza 23 Mei. Wafanyakazi waliogoma wanatakiwa kurudi kazini kesho asubuhi.

Wafanyakazi wa Manispaa ya Oslo bado wako kwenye mgomo. Oslo ni Manispaa, Mkoa na Mji mkuu, hivyo basi wafanyakazi wa Oslo wana makubaliano tofauti kidogo na waajiri wao, ukilinganisha na Manispaa zote za Norway. Unio (Oslo) na KS wameitwa kwa mpatanishi wa migororo ya wafanyakazi na waajiri (Riksmeklingsmannenen) ili kuangalia uwezekano wa mgomo wa Oslo kwisha haraka.


Chanzo cha habari: TV 2 Nyhetskanalen.

No comments: