Thursday, July 31, 2008

Kiula amvaa Chenge



na Kulwa Karedia


ALIYEKUWA Naibu Waziri wa Ujenzi katika serikali ya awamu ya tatu, Nalaila Kiula (pichani), amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumuondoa Mwenyekiti wa Maadili wa chama hicho, Andrew Chenge kwenye wadhifa huo, hadi tuhuma zinazomkabili zitakapopatiwa ufumbuzi.

Mbali ya kumtaka Chenge kuondolewa kwenye wadhifa huo, Kiula pia ametaka viongozi wa juu wa CCM wanaotuhumiwa ufisadi, wasimamishwe mara moja kuhudhuria mikutano yote ya juu ya chama hicho.

Akizungumza na Tanzania Daima katika mahojiano maalum Dar es Salaam jana, Kiula alisema hatua ya Chenge kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Maadili ndani ya CCM huku akikabiliwa na tuhuma za ufisaidi, hakutoi picha nzuri kwa jamii.

“Ni wakati mzuri sasa kwa CCM kuhakikisha wanamweka kando kwanza mwenyekiti wao wa maadili, ndugu Chenge kutokana na tuhuma zinazomkabili kwanza, hadi uchunguzi dhidi yake utakapokamilika,” alisema Kiula.

Alisema kitendo cha CCM kuendelea na kiongozi huyo bila kuchukua hatua zozote, kinaonyesha wazi kwamba vita dhidi ya ufisadi ni ngumu.

“Huwezi kuendesha vita dhidi ya ufisadi kama wale wanaotuhumiwa, ndiyo viongozi wa maadili ndani ya chama, litakuwa jambo la busara kama tukisikia kwamba CCM wamemweka kando hadi uchunguzi utakapokamilika,” alisema Kiula.


Bofya na endelea>>>>>


No comments: