Wanawake wengi wa
Kitanzania waikana
nchi ili kuolewa nje
TAKWIMU za serikali kwa mwaka 2007/08 kuhusu taratibu za uraia zimetoka zikionyesha wanawake wa Kitanzania wanaongoza kwa kuukana uraia wao ili waolewe nje.
Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo
ya Ndani kwa mwaka 2008/09, Waziri Lawrence Masha, alisema katika kipindi cha mwaka
2007/08 jumla ya Watanzania 63 waliukana uraia kati yao wanawake ni 50.
Masha alisema idadi hiyo ni sawa asilimia 74.9 ya walioukana uraia na kuongeza
kwamba wanaume walikuwa 13 sawa na asilimia 20.9.
Kuhusu idadi ya vijana wazamiaji nje, alisema kumekuwa na ongezeko la wazamiaji
hadi kufikia 382 mwaka 2007/8 kutoka 193 mwaka 2006/07.
Alisema wazamiaji hao vijana husingizia kwamba, wanakwenda kutafuta maisha bora
No comments:
Post a Comment