Wednesday, July 30, 2008

Vitisho vya kumalizana miongoni mwa viongozi waandamizi wa siasa na serikali nchini, hali ngumu ya maisha, ushirikina na usfisadi ni mambo ambayo yanamfanya Rais Jakaya Kikwete kuwa njia panda, Uwazi limegundua.

Ugunduzi huo umekuja baada ya wachambuzi wetu wa mambo ya kisiasa kubaini kuwa tangu nchi yetu ipate uhuru haijawahi kutokea viongozi waandamizi wa vyama na serikali kutishia kumalizana hadharani ama kimaisha, kisiasa au hata kiuchumi .

Viongozi ambao anawaongoza waliotishia kufunguliana kesi ni pamoja na Andrew Chenge aliyeahidi kumfikisha katika vikao vya chama, Spika Samuel Sitta kutokana na madai ya kudaiwa kupeleka uchawi bungeni, Basil Mramba na Grey Mgonja waliotishia kumfikisha mahakamani Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbroad Slaa kwa madai ya kuwahusisha na ufisadi.

Uchotwaji wa fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) uliofanywa na vigogo ambao majina yao ni siri kwa vyovyote unamuumiza kichwa rais pia mkataba wenye utata wa Kampuni ya Umeme ya Richmond ni tatizo lingine ambalo limemsababishia kuteua Waziri Mkuu mwingine baada ya aliyekuwa akikalia, Edward Lowassa na mawaziri wawili, Nizar Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha kujiuzulu Februari 7, mwaka huu.

No comments: