Wednesday, July 30, 2008

na

‘uhuru wa kujiua’




Na Rehema Kimvuli

WAZAZI wengi wa Tanzania wamekuwa wakikimbilia kupeleka watoto kusoma katika shule zilizo nje ya nchi hasa Uganda, bila kufuatilia wasifu wa ndani na nje wa shule hizo.

Ukiwauliza kwa nini wanawapeleka watoto wao wadogo, wa kati ya miaka mitano na 18, utaambiwa kuwa ni kwa ajili ya kupata “elimu bora.”

Wazazi wengi wa Tanzania wanaamini Uganda kuna elimu bora zaidi. Kisa? Eti watoto wao wanaporudi nyumbani wanakuwa wanaongea Kiingereza kizuri, tena kilichonyooka na bila kigugumizi!

Hivi tujiulize elimu bora ni kuzungumza Kiingereza au ni kuelewa ulichofundishwa na kukifanyia kazi kwa manufaa yako binafsi najamii?

Sisemi kuwa siyo muhimu kujua kusoma, kuandika na kuongea Kiingereza. Nasema lugha hiyo isiwe sababu ya kuwapeleka watoto nje ya nchi wakiwa bado wanahitaji malezi ya wazazi.

Kuna wafanyakazi wengi waliopo maofisi hapa Tanzania wanaofanya kazi zao kwa ufasaha; hakika kama inavyotakiwa ingawa hawajui Kiingereza kwa ufasaha.

Hata hivyo, wazazi wanaopeleka watoto wao nchini Uganda, sijui kama wamekuwa wakifuatilia maendeleo yao wawapo huko.


No comments: