Tuesday, August 12, 2008

Bibi afariki baada

ya kukwamwa

na tonge la ugali



Na Willy Sumia, Mpanda

MTU mmoja amefariki dunia baada ya kumeza tonge la ugali wa mahindi na kukwama katika koromeo. Aliyefariki dunia ametajwa kuwa anaitwa Asha Seifu (83) mkazi wa Kitongoji cha Majengo namba moja, Kata ya Kawajense mjini Mpanda, mkoani Rukwa.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi katika msiba huo mtoto wa marehemu, Juma Bakari Mwimbula (54) alisema kuwa Agosti 7, mwaka huu marehemu alipika ugali wa saa mbili usiku na kuanza kula na mwanae na mjuu wake na alipomeza matonge tano alianza kulalamika kuwa tonge limemkaba kooni.
Alisema baada ya hapo walimpa maji ya kunywa, lakini baada ya aliendelea kulalamika kuwa tonge hilo linamuumiza hadi kesho yake saa sita mchana alipokata roho na kuzikwa kesho yake alasiri katika makaburi ya Kawajense.

Inadaiwa kuwa ndugu zake walishindwa kumpeleka hospitalini kutokana na kukosa uwezo wa kifedha. Jeshi la Polisi wilayani Mpanda limethibitisha kutokea kwa tatizo hilo na kwamba uchunguzi juu ya kifo hicho unaendelea kufanywa.




No comments: