Monday, August 11, 2008

Raza sasa ataka



ijitenge




na Saada Said

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mfanyabiashara maarufu Zanzibar, Mohammed Raza, ameshauri Zanzibar ijitenge ili kuepusha mzozo wa hadhi ya Zanzibar unaoendelea nchini.

Raza alitoa kauli hiyo nzito jana wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari mjini hapa.

Alisema kutokana na tofauti hizo, kumekuwa na maneno mengi yasiyo ya msingi yanayotolewa na viongozi wa upande wa Bara dhidi ya hadhi ya Zanzibar ambayo hayana nia ya kuimarisha Muungano.

Alisema amesikitishwa na kauli ya hivi karibuni iliyotolewa na mmoja wa makada wa siku nyingi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa bendera ya Zanzibar ni sawa na ya timu ya mpira na wimbo wao wa taifa, hauna tofauti na kwaya.




No comments: