Tuesday, August 19, 2008

Brazil yabamizwa

na Argentina

3 – 0

Naijeria yaiua

Ubelgiji

4 - 1



Lionel Messi wa Ajentina (kushoto) akipena mkono na kubadilishana bendera na Ronaldhino (Brazil) kabla ya mechi ya nusu fainali kwenye uwanja wa Urafiki mjini Beijing 19.8.2008


Messi akimwonyesha Ronaldhino jinsi ya kulisakata kabumbu!


Alex Silva wa Brazil akipiga "tik´taka"


Sergio ARguero (nam. 16) wa Ajentina akifunga goli.


Ronaldhino akionyesha masikitiko baada ya Brazili kufungwa na Ajentina


Chinedu na mwenzake wakifurahia goli la Naijeria. Chinedu aliwahi kuichezea Lyn FC ya Oslo.


Chinedu Ogbuke Obasi akionyesha ufundi wake wa kulisakata soka 19.8.2008


Kocha wa Naijeria Samson Siasia akizungumza na mchezaji wake Solomon Okoronkwo 19.8.2008. Siasia enzi zake alikuwa mchezaji maarufu wa timu ya taifa ya Naijeria


Maarten Martens wa Ubelgiji na Solomon Okoronkwo wa Naijeria 19.8.2008


Tom de Mul wa Ubelgiji 19.8.2008. Picha zote Foto-net.


Argentina kwa mara nyingine tena wameonyesha kuwa ni wababe zaidi ya Brazil kwenye kandanda, baada ya kuifunga Brazil kwa mabao 3 – 0 kwenye nusu fainali za Olimpiki. Argentina wakiongozwa na Messi walicheza soka la ukakika zaidi ya Brazil, ambao walionekana kucheza bila fomesheni yoyote. Kwenye nusu fainali ingine, Naijeria wameingia fainali baada ya kuifunza adabu Ubelgiji kwa kuwafunga magoli 4 – 1.

Fainali itakuwa marudio ya fainali ya Olimpiki mjini Atlanta 1996 kati ya Naijeria na Argentina. Fainali za mwaka huu, Naijeria wanaonyesha kuwa na timu bora zaidi.



No comments: