Wednesday, August 20, 2008

Rais Mwanawasa

wa Zambia

afariki dunia





LUSAKA, Zambia

RAIS wa Zambia, Bw. Levy Mwanawasa (59), amefariki dunia akiwa katika matibabu nchini Ufaransa.

Rais huyo alifariki dunia jana asubuhi, kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Bw. Rupiah Banda ambaye anatarajiwa kukaimu wadhifa huo, aliyezungumza kupitia televisheni ya Taifa hilo.

"Ndugu wananchi, kwa huzuni, ninapenda kuwajulisha kuwa Rais Dkt. Levy Patrick Mwanawasa amefariki asubuhi ya leo, majira ya 4.30," alisema Bw. Banda kama alivyonukuliwa na Shirika la Habari la Reuters.

Alisema," ninapenda kuwajulisha kuwa maombolezo kitaifa yanaanza leo na yatakuwa kwa siku saba."

Mwanawasa alikuwa alianza kuugua kiharusi alipokuwa amekwenda Misri kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mwishoni mwa Juni mwaka huu na alipelekwa Ufaransa ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

No comments: