Monday, August 18, 2008

Brig. Mwakanjuki


ni nchi



na Kulwa Karedia

ALIYEKUWA Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Brigedia Jenerali (mstaafu) Adam Mwakanjuki, ameibuka na kusema Zanzibar ni nchi na anakerwa na wanaopinga ukweli huo.

Mwakanjuki, mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za visiwani Zanzibar, alisema hatua ya baadhi ya watu na viongozi kusema Zanzibar si nchi haina maana, kwani ina kila kitu kinachofanya ijitawale yenyewe.

Akizungumza na Tanzania Daima katika mahojiano maalumu Dar es Salaam, jana, Mwakanjuki alisema Zanzibar ni nchi kamili ambayo haipaswa kujadiliwa kwa vile haoni sababu ya kuanzisha malumbano yasiyo na tija.

“Zanzibar ni nchi na itaendelea kuwa nchi kamili ambayo imejitosheleza kwa kila kitu. Sasa hawa wanaosema si nchi hawana jipya…hii ni dola ukizingatia tuna Rais anayechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na wananchi,” alisema Mwakanjuki.


No comments: