Monday, August 18, 2008


Rais Kikwete

apokea ripoti

ya EPA



Rais Jakaya Kikwete jumatatu alipokea rasmi ripoti ya uchunguzi wa upotevu wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (External Payments Accounts - EPA) katika Benki Kuu (BoT) katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu jumatatu jioni, Rais Kikwete alikabidhiwa ripoti hiyo na Mwenyekiti wa Timu iliyokuwa inafanya uchunguzi huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

Mwanasheria Mkuu huyo alifuatana na wajumbe wengine wa Timu hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hosea.


No comments: