Mbona Rais wetu
Jakaya Kikwete
yu kimya?
Padri Privatus Karugendo
WIKI hii Mchungaji Mtikila amefikishwa mahakamani kwa kosa la uchochezi la kumwita Rais wetu gaidi. Siungi mkono matamshi ya Mchungaji Mtikila, lakini ningependa tuangalie kwa mbali. Tutafakari na kuona jinsi ya kuliokoa taifa letu la Tanzania. Watu wameanza kuwa na mawazo mengi na mengine ya hatari. Kusema kwamba Rais ni gaidi ni dalili za hatari. Nafikiri mawazo haya yote yanachochewa na ukimya wa Rais wetu mpendwa.
Kama nilivyosema kwenye makala yenye kichwa cha habari: “Mafisadi watashinda lakini..”, ni kwamba Rais wetu hatoi mwanga ili tukafahamu yeye yuko upande gani. Yamesemwa mengi, yameibuliwa mengi juu ya ufisadi, lakini hatuoni hatua zikichukuliwa.
No comments:
Post a Comment