Mjadala wa
na Salehe Mohamed, Dodoma
MJADALA wa hadhi ya Zanzibar kama ni nchi au la, umefikia katika hatua mbaya baada ya Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM), kutamka bungeni kuitaka serikali kuvunja muungano huo.
Alisisitiza kuwa ni bora muungano huo uvunjwe, kwa madai kuwa viongozi wa Zanzibar wamechoshwa na muungano kutokana na kauli zao.
Mbunge huyo ametoa kauli hiyo nzito huku Rais Jakaya Kikwete akitarajia kulihutubia Bunge leo na hoja ya hadhi ya Zanzibar, huenda ikawa sehemu ya hotuba yake, kutokana na mvutano mkali unaozidi kuchukua sura mpya kila siku tangu ilipoibuka bungeni.

No comments:
Post a Comment