Friday, August 01, 2008


Ngozi ya mtu kuwa ngazi

ya utajiri? Si giza hii?



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi Frank,


Nakupenda sana mpenzi wangu. Baada ya kusikia jinsi ulivyomhifadhi Mwadawa eti alikuwa anatafutwa kwa kuwa ni albino, wakati polisi wanajidai hawawezi kufanya lolote, wewe mwanamume kweli! Wewe dume langu la kudumu, si kama vile vidume vinavyofikiri kumtwanga mwanamke kama mahindi eti ni udume. Kwa mfano ulimwona kwenye gazeti yule mama aliyechomwa kwa kukataa kumpa mume wake pesa za matumizi. Unamchoma mkeo hadi karibu amekufa. Hivi wanaume wengine wakoje?

Lakini wewe shujaa wangu, damu yangu inasisimka kila nikifikiria ulivyoingilia kati na kumtorosha Mwadawa, Mwadawa mpenzi wetu darasani, Mwadawa mwenye ucheshi wa kila aina, Mwadawa tuliyemtegemea ataenda chuo kikuu siku moja, wanamfuata usiku na kutaka kumchinja, Mwadawa wanataka kumgeuza dawa ya utajiri wa katili au fisadi fulani, haiingii akilini.



No comments: