Rais Kikwete
Rais Jakaya Kikwete amepigilia msumari wa mwisho kwenye mjadala uliochukua wiki kadhaa sasa wa kama Zanzibar ina hadhi ya nchi kwa kusema kuwa kwa masuala ya ndani Zanzibar ni nchi, lakini kwa masuala ya nje, nchi ni Tanzania. Alitoa msimamo huo mjini hapa jana wakati akilihutubia Bunge na Taifa.
Alisema; “Nchi yetu ni moja, watu wake wamoja na Muungano uko imara, haya yaliyozuka ya Zanzibar ni nchi au si nchi tutayamaliza kwa kufuata utaratibu.” Hata hivyo, aliwatahadharisha wanasiasa na hasa viongozi, kuacha kutoa matamshi juu ya suala hilo ambayo yanaweza kugonganisha vichwa vya wananchi. “Kama zipo ajenda nyingine tuziseme, si hili,” alisema Kikwete.
Huku akionyesha kukerwa, Rais Kikwete aliwakemea baadhi ya viongozi wa serikali (hakuwataja) walioko katika Kamati ya pamoja inayoshughulikia namna ya kuondoa kero za Muungano, ambao wako mstari wa mbele katika kuchochea malumbano hayo. Ingawa hakuwataja, baadhi ya viongozi wa Zanzibar waliolishupalia suala hilo la Zanzibar ni Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamuhuna na Waziri wa Nchi katika Ofisi yake, Hamza Hassan Juma.
“Hii si sawa, tunaigawa nchi,” alisema Rais Kikwete huku akipiga marufuku malumbano ya hadharani baina ya viongozi wa pande zote za Muungano juu ya suala la Zanzibar. Alisema inasikitisha kwamba leo hii miaka 44 tangu kufanyika kwa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika baadhi ya viongozi wanashindwa kuelewa kilichokubaliwa baina ya waasisi wake, Mwalimu Nyerere na Abeid Amani Karume.
“Waliunda mamlaka (sovereignty) mpya inayofahamika kama Tanzania. Kwa mambo ya ndani kuna mambo ya nchi ya Zanzibar na sheria, kwa mambo ya nje kuna Tanzania. Tatizo ni nini?” alihoji Rais. Mjadala aliokuwa akiuzungumzia Rais uliibuka baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kujibu swali katika mkutano wa sasa wa 12 wa Bunge unaoendelea hapa Dodoma kwamba Zanzibar si nchi.
Kauli yake hiyo ilisababisha mwangwi wenye mtikisiko wa siasa, hasa kutoka kwa baadhi ya mawaziri na wajumbe wa pande zote wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Akirejea mazungumzo ya Mwafaka wa siasa kati ya CCM na CUF ambayo sasa yamekwama, Rais Kikwete alisema jitihada zinazofanywa ni kuyanasua mazungumzo hayo yalipokwama, ingawa alikiri kuna uzito hasa kutokana na pande zote kuwa na kiwango kikubwa cha kutoaminiana. Alisema yeye na serikali yake hawajakata tamaa na matarajio ni kuhakikisha ifikapo mwakani mazungumzo hayo yawe yamekamilika.
Kutoka: HabariLEO Ijumaa 22.08.2008

1 comment:
The IMF eliminate food and fuel subsidies for the poor in Indonesia. At the same time the IMF soaked up tens of billions of dollars to save Indonesia's financiers or rather the international banks from whom they had borrowed.
A document leaks out of the World Bank, called, "Master Plan for Brazil." In it it spells out five requirements to ensure a flexible public sector workforce. These are as follows:
Reduce Salary/Benefits
Reduce Pensions
Increase Work Hours
Reduce Job Stability
Reduce Employment
1999 In Brazil, Rio's privatized electric company named, "Rio Light," is responsible for repeated blackouts in neighborhoods. The company blames the weather in the Pacific Ocean for the blackouts, when Rio is on the Atlantic. The blackouts wouldn't have anything to do with the fact that after privatization Rio Light axed 40% of the company's workforce would it? No problem for Rio Light, as a result of that their share price went up 33%.
2000 The IMF require Argentina to cut the government budget deficit from its current $5.3 billion to $4.1 billion the following year, 2001. At that point unemployment was running at 20% of the working population. They then upped the ante and demanded an elimination of the deficit. The IMF had some ideas of how this could be achieved. Cut the government's emergency employment program from $200 a month to $160 a month.
They also asked for an across the board 12 - 15% cut in salaries for civil servants and the cutting of pensions to the elderly by 13%. By December of 2001, middle class Argentineans sick of literally hunting the streets for garbage to eat, started burning down Buenos Aires. In January Argentina devalued the Peso wiping out the value of many common people's savings accounts. Dismayed that they can't rape that country further, James Wolfensohn, President of the World Bank, states,
"Almost all major utilities have been privatized."
How do they control the unrest within the population? Let me see, an Argentinean bus driver, a thirty seven year old father of five, lost his job as a bus driver from a company that owed him 9 months pay. During a demonstration against this and other injustices perpetrated upon him and the population, the military police shot him dead with a bullet through the head.
In Tanzania with approximately 1.3 million people dying of AIDS, the World Bank and the IMF decided to require Tanzania to charge for what were previously free hospital appointments. They also ordered Tanzania to charge school fees for their previously free education system then expressed surprise when school enrolment dropped from 80% to 66%.
The IMF and World Bank have been in charge of Tanzania's economy since 1985 during which time Tanzania's GDP dropped from $309 to $210 per capita, standards of literacy fell and the rate of abject poverty increased to envelop 51% of the population.When the IMF and World Bank took charge in 1985, Tanzania was a socialist nation. In June 2000 the World Bank reported arrogantly,
"One legacy of socialism is that most people continue to believe the State has a fundamental role in promoting development and providing social services."
There is rioting in Bolivia after the World Bank drastically increase the price of water. The World Bank claim this is necessary to provide for desperately needed repairs and expansion. This is poppycock, my own water supplier is Wessex Water, a privatized water company that was actually owned by Enron! Since privatization (England was the first country to privatize the public water supply), the quality dropped and the prices exploded.
Almost all privatized water companies in Britain have consistently failed to meet government targets on leakages.
Post a Comment