WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amesema malumbano yanayoendelea sasa kuhusu hadhi ya Zanzibar, hayawezi kumalizika kwa kuunda serikali tatu, kwani muundo huo hautafanya kazi vizuri, kwa kuwa Zanzibar ni nchi ndogo.
Sumaye alisema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na kipindi cha ‘Jicho Letu Wiki Hii’, kinachorushwa na kituo cha Radio Clouds, cha jijini Dar es Salaam. Sehemu ya pili ya mahojiano hayo itarushwa Jumamosi ijayo na kituo hicho cha redio.

No comments:
Post a Comment