Vihiyo si Bongo tu
hata Norway wapo!
Vyuo vingi hapa Norway vimekuwa vikigundua wanafunzi kadhaa wanaoghushi shahada za kwanza na uzamili ili kujiunga navyo. Chuo Kikuu Oslo (the University of Oslo), Chuo Cha Biashara (Norwegian School of Management) na Chuo Cha Oslo (Oslo University College) vimekuwa vikikamata wanafunzi kama watano kwa mwaka kila kimojawapo. Wanaoghushi vyeti ni Wanorweji na wengine kutoka nje ya Norway.
NOKUT (The Norwegian Agency for Quality Assurance in Education) wanasema kuwa tatizo la kughushi vyeti ni kubwa na linaongezeka kila siku. Watu 30 wamegunduliwa kwa kughushi vyeti toka mwaka 2005 NOKUT ilipoanzishwa..
Kabla ya muhula wa masomo kuanza Wiki mbili zilizopita, dada mmoja amekamatwa kwa kughushi vyeti toka ”Trinity College and University in Spain”. Dada huyo amekiri kosa kuwa alinunua shahada ya kwanza na ya uzamili kwenye mtandao kwa Paundi za Kiingereza 125 na 195. Tayari ameshafikishwa mahakamani. Kesi imesikilizwa kwa mara ya kwanza jana kwenye mahakama ya mwanzo ya Manispaa ya Asker na Baerum, mkoa wa Akershus.
1 comment:
Kati ya wageni waliogunduliwa kughushi vyeti, hakuna Mbongo?
Post a Comment