Na Gaudence Massati
SUALA la Zanzibar kuwa nchi ama la linazidi 'kuwapandisha presha'Wazanzibari na sasa baadhi yao wanahoji iwapo Muungano wa 1964 ulilenga kuuza kisiwa hicho kwa Tanganyika.
Aidha wameeleza kuwashangaa wabunge wa Zanzibar walio kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano na kuhoji bado wanaendelea kufanya nini wameambiwa hawana nchi.
Akizungumza kwa njia ya simu jana kutoka Zanzibar, aliyewahi kuwa Mshauri wa Rais wa Zanzibar, Bw. Mohamed Raza, alisema kwa hali ilivyosasa kuna maswali mengi ambayo Wazanzibari wanahitaji majibu ili kujiridhisha na hoja inayoendelea.
"Wabunge hawa wangekuwa watu jasiri,wapo kwa maslahi ya Wazanzibar,bila shaka wangerudi kwa sababu wanamuwakilisha nani sasa, wakati wameambiwa kuwa Zanzibar si nchi !"Alihoji Bw. Raza.

No comments:
Post a Comment